▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼
MTU mmoja amefariki dunia kwa kuangikuwa na ukuta na nyumba kadhaa kubomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Manispaa ya Zanzibar.
Kamanda Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Mkadam Khamis, alimtaja mtu aliyefariki dunia kuwa Salim Mohamed, mkazi wa Migombani ambaye aliangukiwa na ukuta nyumbani kwake alfajiri kuamkia jana.
Kamanda Mkadam alifafanua kuwa Salim alitoka nje ya nyumba yake kuangalia mazingira ya mvua zilizokuwa zikinyesha, lakini ghafla ukuta ulibomoka na kumuagukia na kusababisha kifo chake.
Post a Comment