Loading...

BREAKING NEWS: TAARIFA KUTOKA IKULU MUDA SI MREFU..RAIS MAGUFULI KIBOKO AFANYA UTEUZI WA HATARI AMBAO HAUKUTARAJIWA KWA JAPAN KUPATA BALOZI WA TANZANIA

▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.

Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.

Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo Ia Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dares salaam
18 Aprili 2016


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright bongonews | Designed By JAMIIYETUBONGO.COM
Back To Top