▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼
Mahakama ya Mkoa wa Mwanza imetengua ushindi wa madiwani watatu wa Chadema Jijini Mwanza kufuatia ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura uliofanywa na tume ya Uchaguzi mwishoni mwa mwaka Jana.
Kata mbili kati ya hizo ambayo ni kata ya Isamilo, na Kata ya Kitangiri marejeo ya Uchaguzi yatafanyika haraka iwezekanavyo Mara baada ya tarehe ya Uchaguzi kutangazwa na tume wakati kata ya Nyamanolo Diwani wa CCM ametangazwa kuwa mshindi Mara baada ya kuhujumiwa kwa kuibiwa kura.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu amesema kuwa Mahakama imefanya maamuzi ya kidemokrasia hivyo amewahakikishia ushindi wa kishindo wafuasi wa chama hicho kwenye kata zitakazorudiwa Uchaguzi
Post a Comment