Loading...

SUMATRA yatangaza nauli kwa mabasi yaendayo kasi

▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼
Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA), leo hii (May 09 2016) SUMATRA imetangaza nauli hizo.

SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa ni 800 na mwanafunzi 200.

Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili mfululizo na ifikiapo May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.

Msimamizi wa mradi kutoka DART, Injinia Ronald Lwakatare amesema haya wakati akiongea na waandishi wa habari mchana huu;

‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright bongonews | Designed By JAMIIYETUBONGO.COM
Back To Top