▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Millen Magese ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni Jijini Dar es Salaam, amendika ujumbe kwa watanzania akiwaambia kuwa na upendo na kuthamini vya kwao, pamoja na kuvitangaza, huku akielezea matamanio yake ya kwenda mbuga ya wanyama ya Serengeti na Saadani.
“Tuwe na utamaduni wa kupenda vya kwetu na kusifia vya kwetu, na kutangaza vya kwetu......Tanzania is beautiful ..... Tutembelee vya kwetu .#SmallVacayInTanzania, next....wish to go to Serengeti and Saadani, #TakingTimeOff”, aliandika Millen Magese.
Kwa sasa mwanamitindo huyo yupo kwenye kampeni kubwa ya kutafuta tiba ya ugonjwa wa endometriosis, ambao umemsumbua kwa miaka 13 mpaka sasa, uliopelekea kufanyiwa upasuaji mara 13 kupata matibabu yake.
Post a Comment