Loading...

HABARI YA HIVI PUNDE: UKAWA SASA BALAA MEYA KINONDONI AGEUKA TISHOO ATUMBUA MAJIPU MAZITO YALIOACHWA KUTUMBULIWA NA KUWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI HAWA...

▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼

Matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana.
Madiwani la Manispaa ya Kinondoni wakiwasimamishakazi Mahenge na Chidaga baada ya kubainika kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha hasara ya kwa manispaa hiyo.
Uamuzi wa kuwasimamisha kazi maofisa hao yalitokana na maazimio ya kikao cha baraza hilo kilichokaa juzi.
Akisoma maazimio ya baraza hilo mbele ya waandishi wa habari na wajumbe wa baraza hilo jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob, alisema katika kikao cha Kamati ya Fedha na Uongozi cha Aprili 29, mwaka huu kiliagiza kuorodheshwa kwa mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na mwanasheria huyo na baada ya kugundua makosa hayo baraza liliamua kuwasimamisha kazi.
Alisema baadhi ya makosa ambayo yaligundulika ni pamoja na mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa, ambao manispaa ilipaswa kupata Sh. milioni 900 kwa mwaka, lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba mapato hayajawahi kulipwa na hivyo kupoteza Sh. bilioni 4.5 hadi sasa.
Mwingine ni mgogoro wa wapangaji wa nyumba za Magomeni Kota, ambao manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo hilo na kuwaondoa wapangaji hao waliokuwa wanaishi katika nyumba hizo ambao waliamua kufungua kesi mahakamani kupinga kuondolewa katika nyumba hizo wakidai kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia.
Alisema kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hilo, mahakama iliamuru manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama na hivyo halmashauri kuamua kutengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji hao Sh. 1,080,000 kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja.
Alisema kutokana na mgogoro huo manispaa inatakiwa kulipa Sh. 3,271,520,000 kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa Sh. 695,520,000, ambalo ni pango la mwaka pamoja na kulipa Sh. 2,576,000,000 ambayo ni fidia ya viwanja 644.
Sababu nyingine ya kusimamishwa kwa maafisa hao ni kutokana na sakata la uwekezaji katika ufukwe wa Coco Beach Oysterbay, ambalo manispaa iliingia mkataba na Q - Consult Limited na ikashindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na manispaa ikavunja mkataba huo.
Hata hivyo kambuni hiyo haikuridhika na hivyo kufungua kesi mahakamani ambayo nayo haikusimamiwa vizuri ikiwamo kushindwa kufika kwenye kesi na hivyo kushindwa kesi.
Kadhalika, alisema sababu nyingine ni mradi wa ujenzi wa maduka ya Makumbusho (Eastern Capital Ltd) ambayo mkataba wake amabo pia ni wa uendeshaji wa stendi yake pia ulionekana kutokuwa na manufaa kwa halmashauri, huku ikipata asilimia moja tu ya makusanyo kwa mwaka sawa na Sh. milioni nne tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, wakati inatumika stendi ya kawaida ya zamani halmashauri hiyo ilikuwa ikipata Sh. milioni 12 kwa mwezi.
Kwa upande wake,Meya wa jiji la Dar es amemsimamisha Iddy, baada ya kubaini kuwapo kwa changamoto nyingi ikiwamo, utaratibu wa ukusanyaji wa ushuru katika stendi hiyo.
Aidha, alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, kuvunja mkataba wa mkandarasi anayefanya usafi katika kituo hicho mara moja kutokana na kushindwa kufanya usafi kikamilifu na kutangaza tenda ya kumpata mkandarasi mwingine.
Maagizo hayo aliyatoa wakati Baraza la Madiwani la jiji lilipofanya ziara ya kutembelea miradi yake katika kituo hicho, Dampo la Pugu na eneo la mtambo wa lami, Tabata.
“Kuanzia leo meneja wa kituo hiki cha mabasi naagiza apangiwe majukumu mengine wakati tunatafuta utaratibu wa kumpata meneja wa kusimamia kituo hiki,” alisema Mwita.
Pia alimtaka meneja huyo kuipa ushirikiano kamati iliyoundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika kituo hicho cha mabasi, kabla hajaanza kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa.
Mwita pia alimuagiza Mwanasheria wa jiji kuangalia utaratibu wa kubadili mkataba waliyoingia na Mradi wa Mabasi ya kwenda haraka jijini hapa (Dart), kwa ajili ya kutoa asilimia 52 ya kituo hicho ilia kujenga ghala.
Imeandikwa na Elizabeth Zaya na Na Mary Geofrey

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright bongonews | Designed By JAMIIYETUBONGO.COM
Back To Top